Kongamano la Taifa la Wadau wa Sekta ya Afya kuhusu Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
09 Jul, 2024
Kongamano la Taifa la Wadau wa Sekta ya Afya kuhusu Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo limefanyika leo tarehe 6 Julai, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kongamano hili ni moja ya mwendelezo wa makongamano yanayowakutanisha wadau wa sekta mbali mbali nchini ili kutoa maoni yao kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayoratibiwa Tume ya Mipango.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Wizara ya Afya chini ya Waziri wake, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo huku Mgeni rasmi katika kongamano hilo akiwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb).