Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma za ununuzi, uhifadhi na ugavi wa bidhaa na huduma kwa Tume.
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa Mpango wa Ununuzi wa Mwaka.
- Kutoa ushauri wa masuala ya ununuzi wa bidhaa na huduma na usimamizi wa vifaa.
- Kupanga na kusimamia ununuzi na uondoaji wa vitu kwa kuzingatia taratibu za zabuni za taasisi isipokuwa kutoa uamuzi na mkataba.
- Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni na kuandaa ripoti za kila mwezi.
- Kutoa huduma ya sekretarieti kwenye Bodi ya Zabuni.
- Kuandaa taarifa za mahitaji.
- Kuandaa nyaraka za zabuni.
- Kuandaa matangazo ya fursa za zabuni.
- Kuandaa nyaraka za mkataba na kutoa nyaraka za mkataba zilizoidhinishwa.
- Kutunza nyaraka za ununuzi.
- Kutunza rejista ya mikataba yote iliyotolewa.
Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja