Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

Idara ya Maeneo Muhimu ya Matokeo ya Taifa

Lengo

Kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa maendeleo ya utekelezaji wa programu za Maeneo Muhimu ya Kitaifa (NKRAs).

Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:

    1. Kuwezesha utambuzi wa NKRAs,
    2. Kuratibu na kuwezesha utekelezaji wa programu za NKRA,
    3. Kuandaa mara kwa mara taarifa za utekelezaji wa mipango na miradi ya NKRAs;
    4. Kuchanganua na kuthibitisha taarifa za utekelezaji kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma yanayotekeleza miradi;
    5. Kutoa ushauri na suluhisho la kutatua changamoto zinazokabili utekelezaji wa mipango ya NKRAs;
    6. Kutoa ushauri elekezi na kuishauri Serikali kuhusu NKRAs;
    7. Kupanga na kuendesha shughuli za labs;
    8. Kuwezesha uandaaji wa mikataba ya utendaji wa Mawaziri wanaohusika katika programu na miradi iliyo chini ya Wizara zao;
    9. Kuwezesha uandaaji wa viashiria muhimu vya utendaji vya Taifa na Wizara vya programu na miradi; na
    10. Kufanya tathmini huru za utendaji wa Wizara mbalimbali katika NKRAs.

 Idara itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:

  1. Sehemu ya Maeneo Muhimu ya Taifa ya Matokeo ya Uchumi (NEKRAs); na
  2. Sehemu ya  Maeneo Muhimu ya Taifa ya Matokeo ya Jamii (NSKRAs).