Idara ya Ubunifu, Tafiti na Maendeleo
Lengo
Kubaini na kuchanganua maeneo ya ubunifu wa nchi na kushauri kuhusu maeneo ya utafiti kwa ajili ya kuchochea maendeleo endelevu.
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kubuni mikakati ya kuanzisha sayansi na teknolojia ya uvumbuzi nchini;
- Kukuza mbinu za ubunifu katika mipango ya maendeleo na utekelezaji;
- Kubaini na kufanya utafiti wa jambo lolote ambalo Tume inaona lina manufaa kwa uchumi;
- Kuhakikisha uwezo wa rasilimali kupitia tafiti, mapitio na tathmini za mara kwa mara kwa madhumuni ya utekelezaji endelevu wa mipango ya maendeleo ya kitaifa;
- Kushirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa za utafiti na taaluma katika masuala ya tafiti;
- Kuchanganua na kusambaza matokeo ya tafiti; na
- Kuandaa miongozo ya tafiti inayohusiana na maendeleo ya uchumi-jamii.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Ubunifu; na
- Sehemu ya Tafiti na Maendeleo