Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

Kitengo cha Fedha na Uhasibu

Lengo

Kutoa huduma bora za usimamizi wa fedha na uhasibu.

Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kuandaa Taarifa za Fedha za Robo Mwaka, Nusu Mwaka na Mwaka;
  2. Kukagua Vocha za Malipo na nyaraka zinazoambatana nazo ili kuzingatia Sheria za Usimamizi wa Fedha;
  3. Kuratibu na kujibu hoja za ukaguzi zinazoibuliwa;
  4. Kushughulikia malipo ya fedha taslimu na kutunza nyaraka za fedha;
  5. Kuandaa malipo ya mishahara na kuhakikisha makato yote ya kisheria yanatumwa kwa wakati kama inavyoelekezwa; na
  6. Kuandaa, kufanya malipo na kufuatilia matumizi.

Kitengo hiki kitaongozwa na Mhasibu Mkuu.