Idara ya Ufuatiliaji wa Utendaji na Tathmini
Lengo
Kubaini thamani ya fedha na matokeo ya uwekezaji wa umma kwa maendeleo ya nchi.
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango ya taifa,
- Kufuatilia na kutathmini miradi ya kielelezo na kupima utekelezaji wa miradi hiyo;
- Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu masuala ya mipango na usimamizi wa uchumi;
- Kuchanganua na kuthibitisha taarifa za utekelezaji kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma yanayotekeleza miradi;
- Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mara kwa mara ya utekelezaji na kuandaa taarifa za utekelezaji;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Wizara, Mipango ya Mwaka na Programu mbalimbali;
- Kuanzisha michakato ya ufuatiliaji na tathmini katika Utumishi wa Umma; na
- Kutoa taarifa za kitakwimu wakati wa kuandaa mipango na bajeti.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:-
- Sehemu ya Mifumo na Kujenga Uwezo; na
- Sehemu ya Miradi ya Taifa.