Idara ya Mipango na Bajeti
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma bora za mipango, bajeti, tafiti, uvumbuzi na utoaji wa taarifa za utendaji.
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kufanya kazi za mpango mkakati wa Tume, ikiwa ni pamoja na kuandaa Mipango Mkakati, Mipango ya Mwaka, Bajeti na miradi ya maendeleo;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango mikakati ya muda wa kati, bajeti, mipango kazi na miradi ya maendeleo;
- Kufanya tathmini za mara kwa mara za utendaji kazi na kuandaa taarifa;
- Kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Tume;
- Kuhifadhi takwimu za Tume;
- Kupanga na kupitia miradi ya maendeleo;
- Kuratibu masuala ya Bunge;
- Kuratibu shughuli za tafiti na ubunifu katika Tume;
- Kufanya utafiti wa Huduma zinazotolewa na Tume
- Kukusanya, kupitia, na kuchanganua data, takwimu, na taarifa za shughuli za Tume, na
- Kuanzisha mpango mkakati na mchakato wa bajeti ya Tume.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Mipango na Bajeti; na
- Sehemu ya Tafiti na Ubunifu.