Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Lengo

Kutoa utaalamu na huduma za habari, mawasiliano na kuzungumza na umma na vyombo vya habari.

Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano wa Tume;
  2. Kufanya uchanganuzi wa wadau na kuchunguza ujumbe;
  3. Kutafiti masuala yanayoibuka kutokana na utekelezaji wa mipango ya kati na ya muda mrefu na kuandaa majibu;
  4. Kuwezesha ushirikishwaji wa umma katika programu za Tume;
  5. Kuongeza uelewa wa umma  kuhusu majukumu na shughuli za Tume;
  6. Kuratibu mikutano ya waandishi wa habari na Tume;
  7. Kuratibu na kuchangia maudhui ya tovuti ya Tume;
  8. Kuratibu maandalizi na utayarishaji wa makala na majarida ya Ofisi;
  9. Kuwa kiunganishi kati ya Tume na Taasisi zingine za Serikali na umma kwa ujumla;
  10. Kuandaa na kusambaza taarifa kwa umma kuhusu sera, programu na mageuzi yanayofanywa na Tume;
  11. Kufanya ufuatiliaji na uchanganuzi wa Vyombo vya Habari;
  12. Kusimamia na kuhuisha Tovuti ya Tume; na
  13. Kuratibu na kusimamia ushiriki wa Tume katika Maonyesho ya Kitaifa na Kimataifa.

Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja.