Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Lengo
Kutoa huduma za ushauri kwa Afisa Masuuli kuhusu utekelezaji wa mfumo wa udhibiti wa ndani.
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa na kutekeleza mipango ya ukaguzi ya mwaka na ukaguzi wa kimkakati wa vihatarishi,
- Kupitia na kutoa ripoti ya udhibiti wa stakabadhi, utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha zote za Tume;
- Kupitia na kutoa ripoti ya kuzingatia taratibu za kifedha na uendeshaji zilizowekwa katika sheria au kanuni au maelekezo yoyote ya udhibiti wa matumizi;
- Kuandaa taratibu za ukaguzi ili kuendana utekelezaji wa viwango vya kimataifa;
- Kupitia na kuripoti kuhusu usahihi wa taarifa za fedha na uendeshaji zilizotumika wakati wa uandaaji wa taarifa za fedha na ripoti zingine;
- Kupitia na kuripoti kuhusu mifumo inayotumika kulinda mali, na kuthibitisha uwepo wa mali hizo;
- Kupitia na kuripoti kuhusu shughuli au programu ili kuthibitisha iwapo matokeo yanaendana na malengo yaliyowekwa;
- Kupitia na kutoa ripoti ya hatua zilizochukuliwa na uongozi kuhusiana na ripoti za Ukaguzi wa Ndani na Nje, na kuusaidia uongozi katika utekelezaji wa mapendekezo; na
- Kupitia na kutoa ripoti ya mapungufu ya udhibiti katika mifumo ya kompyuta.
Kitengo hiki kitaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani.