Idara ya Mipango ya Taifa
Lengo
Kufikia ukuaji sawa wa uchumi na uthabiti endelevu wa uchumi-jumla.
Majukumu
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa dira ya taifa ya maendeleo, mipango ya maendeleo ya muda mrefu na ya kati na kusimamia utekelezaji wake;
- Kufanya tathmini ya mara kwa mara na uchanganuzi wa vigezo muhimu vya kiuchumi ikijumuisha uwiano wa malipo, ugavi wa fedha na bei, madeni ya taifa na kuishauri Serikali ipasavyo;
- Kutathmini sera mbalimbali zilizopo kwa lengo la kuboresha utekelezaji wake katika mipango ya maendeleo na kupendekeza sera mpya pale inapolazimu kwa maslahi ya taifa;
- Kusimamia maandalizi ya mipango mikakati ya Kisekta na kuoanisha na mipango ya taifa;
- Kuishauri Serikali kuhusu mabadiliko yoyote katika mipango ya taifa iliyoidhinishwa,
- Kubaini na kuchanganua mahitaji na mikakati ya sekta za miundombinu na huduma;
- Kusimamia na kutoa mwongozo wakati wa kuandaa mipango mikakati inayoandaliwa na wizara, idara zinazojitegemea, wakala, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa;
- Kuendeleza na kukuza utaalamu wa masuala ya uchumi, mipango, takwimu na utaalamu mwingine wa aina hiyo;
- Kuitisha na kuwezesha majukwaa maalumu ya mashauriano ya wadau muhimu katika uandaaji na utekelezaji wa mipango ya taifa.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu nne (4) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Uchumi-Jumla;
- Sehemu ya Miundombinu na Huduma;
- Sehemu ya Sekta za Uzalishaji; na
- Sehemu ya Sekta za Jamii.