Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

Ofisi ya Naibu Katibu Mtendaji - Mipango ya Taifa

Lengo
Kutoa huduma za utaalamu na usaidizi katika Ofisi ya Mipango ya Taifa.

Majukumu 
Majukumu ya Ofisi hii ni kama ifuatavyo: -

  1. Kuandaa dira ya maendeleo ya taifa, mipango ya maendeleo ya muda mrefu na ya kati na kusimamia utekelezaji wake;
  2. Kutathmini utekelezaji wa sera mbalimbali zilizopo za maendeleo ya  uchumi-jamii;
  3. Kusimamia uwiano wa mipango ya kisekta dhidi ya mipango ya kitaifa na matumizi bora na yenye uwiano ya rasilimali za nchi;
  4. Kuishauri Serikali kuhusu mabadiliko yoyote yanayojitokeza katika mpango wa taifa ulioidhinishwa;
  5. Kusimamia na kutoa mwongozo wakati wa kuandaa mipango mikakati inayoandaliwa na wizara, idara zinazojitegemea, wakala, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa;
  6. Kuendeleza na kukuza utaalamu wa masuala ya uchumi, mipango, takwimu na utaalamu mwingine wa aina hiyo; 
  7. Kuitisha na kuwezesha majukwaa maalumu ya mashauriano ya wadau muhimu katika uandaaji na utekelezaji wa mipango ya taifa kwa lengo la kujadili masuala ya mipango hiyo; na
  8. Kufanya tathmini ya mara kwa mara na uchanganuzi wa vigezo muhimu vya kiuchumi ikijumuisha uwiano wa malipo, ugavi wa fedha na bei, madeni ya taifa na kuishauri Serikali ipasavyo.

Ofisi hii itaongozwa na Naibu Katibu Mtendaji na itakuwa na Idara moja.