Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma za usimamizi wa rasilimali watu na kiutawala kwa Tume.
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kutafsiri Sheria ya Utumishi wa Umma, Kanuni za Utumishi wa Umma na Sheria zingine za kazi;
- Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha maadili kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuzuia rushwa;
- Kusimamia utekelezaji wa shughuli kama vile kuajiri, uteuzi, semina elekezi, mafunzo, upandishaji vyeo, nidhamu, kuhakikisha wafanyakazi hawaondoki au kuacha kazi, motisha, kusimamia utendaji na ustawi wa wafanyakazi kwa jumla;
- Kuhakikisha matumizi na usimamizi wa rasilimali watu ulio bora na wenye ufanisi;
- Kuratibu masuala ya Baraza la Wafanyakazi na Vyama vya Wafanyakazi;
- Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa sera, utaratibu na miongozo madhubuti ya kuajiri, mafunzo, kuhakikisha wafanyakazi hawaondoki au kuacha kazi, upandishaji vyeo na kusimamia utendaji kazi;
- Kufanya ukaguzi wa rasilimali watu, mahitaji na ujuzi unaotakiwa;
- Kutoa huduma za usajili, usimamizi na utarishi; na kusimamia kumbukumbu za Ofisi;
- Kushughulikia masuala ya itifaki;
- Kuwezesha utoaji wa huduma za usalama, usafiri na mahitaji ya jumla;
- Kuwezesha matengenezo ya vifaa vya Ofisi, majengo na eneo la ofisi;
- Kuratibu utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha maadili kwa wafanyakazi;
- Kuratibu utekelezaji wa masuala uanuwai; na
- Kuratibu utekelezaji wa Ushiriki wa Sekta Binafsi, uboreshaji wa Utendaji Kazi na Mkataba wa Huduma kwa Wateja.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu; na
- Sehemu ya Utawala.