Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

Utangulizi

Serikali imeunda Tume ya Mipango kupitia Sheria ya Tume ya Mipango ya mwaka 2023 ili kuratibu mipango ya kitaifa.Tume hii ipo chini ya Ofisi ya Rais  kama Mshauri, itafanya kazi kama mtandao wa wataalamu wenye ustadi mzuri katika masuala ya mipango, utafiti, uvumbuzi, ufuatiliaji wa utendaji na tathmini.

Tume ya Mipango itakuwa na jukumu la kupanga mipango ya muda mrefu, ufuatiliaji wa utendaji na tathmini; kufanya utafiti, kuchanganua na kushauri juu ya sera za kisekta, masuala ya maendeleo ya uchumi-jamii na masuala ya sera ya sasa ya  uchumi-jamii sambamba na mwelekeo wa sera itakayofuata. Kwa hiyo, Tume ya Mipango itafanya uchanganuzi wa sera wa kina,  wa kiubunifu na wa kisayansi kuhusu changamoto kuu mbalimbali zinazokabili umma ili kutoa masuluhisho yayotekelezwa na Serikali.