Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kutoa maeneo wakati wa kuandaa mipango na shughuli za programu kwa Tume;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango ya Mwaka na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Tume;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Maeneo Muhimu ya Matokeo ya Kitaifa (NKRA) yaTume;
- Kuwezesha ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi mbalimbali kwa kuandaa nyenzo na violezo vya ripoti kulingana na Viashirio Muhimu vya Utendaji;
- Kufanya tathmini za haraka za mipango ya Tume ili kufanya uamuzi sahihi kuhusu uboreshaji wa programu/mradi na maendeleo kusudi kufikia malengo ya Tume;
- Kufanya tathmini za matokeo ya mafanikio ya Tume dhidi ya Viashirio muhimu vya Utendaji vilivyowekwa;
- Kuimarisha uwezo wa ndani wa Tume wa M&E kupitia mafunzo na na kukuza uelewa;
- Kuandaa mfumo wa M&E wa Tume ikihusisha kuandaa na kutekeleza mwongozo wa M&E; na
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya tathmini ya ndani na nje.
Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja