Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

Idara ya Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na Biashara

Lengo

Kutoa utaratibu mzuri wa ushindani wa sekta binafsi kwa lengo la kupata manufaa dhahiri kutokana na biashara ya nje na ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa.

Majukumu

Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kuchanganua hali ya biashara ya kimataifa na kushauri kuhusu uandaaji sera na mikakati ili kukuza biashara ya nje;
  2. Kutoa mwongozo wa mahusiano ya kiuchumi na nchi zingine, mashirika ya kikanda na kimataifa;
  3. Kuandaa mikakati ya kibiashara ya mazungumzo ya sera na nchi nyingine, mashirika ya kikanda na kimataifa;
  4. Kushauri kuhusu mikataba ya biashara baina ya nchi na nchi nyingi;
  5. Kuwezesha ushirikishawaji wa sekta binafsi katika kusaidia mipango ya maendeleo na utekelezaji;
  6. Kufuatilia, kutathmini na kuchanganua mwenendo wa uchumi na maendeleo duniani na kutathmini athari zake kwa uchumi wa ndani; na
  7. Kutathmini matokeo ya misaada ya nje kwa maendeleo ya uchumi na kushauri ipasavyo.

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:

  1. Sehemu ya Ushirikishaji Sekta Binafsi
  2. Sehemu ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi.