Ofisi ya Naibu Katibu Mtendaji — Ufuatiliaji wa Utendaji na Tathmini
Lengo
Kuhakikisha matumizi bora na yenye ufanisi ya rasilimali za taifa kwa maendeleo.
Majukumu
Majukumu ya Ofisi hii ni kama ifuatavyo:
- Kutathmini hali ya rasilimali za taifa na kuishauri Serikali kuhusu matumizi bora ya rasilimali hizo;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango ya taifa;
- Kufuatilia na kutathmini miradi ya kielelezo na kupima utekelezaji wa miradi hiyo;
- Kuchanganua na kuthibitisha taarifa za utekelezaji kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma yanayotekeleza miradi;
- Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mara kwa mara ya utekelezaji na kuandaa taarifa za utekelezaji;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Wizara, Mipango ya Mwaka na Programu mbalimbali;
- Kuandaa utaratibu wenye ufanisi na jumuishi wa taifa wa ufuatiliaji na tathmini;
- Kupendekeza maeneo ya kuendeleza miradi ya vielelezo na programu kwa ajili ya utekelezaji wake kulingana na dira na mikakati ya maendeleo ya taifa;
- Kuratibu utambuzi wa NKRA;
- Kuratibu utekelezaji wa programu za NKRA;
- Kufuatilia utekelezaji wa Maeneo Muhimu ya Matokeo ya Kitaifa ya sekta mbalimbali za uchumi;
- Kutoa taarifa za utekelezaji wa programu na miradi ya NKRA.
Ofisi hii itaongozwa na Naibu Katibu Mtendaji na itaundwa na Idara mbili (2) kama ifuatavyo:
- Idara ya Maeneo Muhimu ya Matokeo ya Kitaifa; na
- Idara ya Ufuatiliaji wa Utendaji na Tathmini.