Ofisi ya Naibu Katibu Mtendaji - Biashara na Ubunifu
Lengo
Kutoa huduma za utaalamu na usaidizi Ofisini katika masuala ya biashara, uvumbuzi, maendeleo na uhusishaji wa sekta binafsi.
Majukumu ya Ofisi hii ni kama ifuatavyo: -
- Kusimamia maendeleo ya ubunifu katika sayansi na teknolojia nchini;
- Kusimamia mbinu za ubunifu katika mipango ya maendeleo na utekelezaji;
- Kusimamia shughuli za utafiti wa jambo lolote ambalo Tume inaona ni muhimu kwa manufaa ya kiuchumi;
- Kutoa mwongozo wa uhusiano wa kiuchumi na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa;
- Kuchanganua hali ya nchi katika biashara ya kimataifa na kushauri kuhusu sera na mikakati inayofaa kukuza biashara ya nje;
- Kushauri juu ya mikataba ya biashara ya nchi mbili na ya kimataifa; na
- Kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika kusaidia mipango ya maendeleo na utekelezaji.
Ofisi hii itaongozwa na Naibu Katibu Mtendaji na itaundwa na Idara mbili (2) kama ifuatavyo:
- Idara ya Ubunifu, Tafiti na Maendeleo; na
- Idara ya Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na Biashara.