DIRA NA DHIMA
DIRA
Tanzania ya sasa yenye ustawi kiuchumi, kijamii, kisiasa, kimazingira na matarajio bora zaidi siku zijazo.
DHIMA
Kupanga kwa ubunifu ili kuimarisha usimamizi wa uchumi jumuishi na wa mageuzi kupitia fikra za pamoja na utekelezaji ulioratibiwa kwa ustawi wa taifa.
MAADILI YA MSINGI
Tume ya Mipango inaongozwa na maadili ya msingi sita (6) katika utendaji kazi ambayo ni:
MAADILI YA MSINGI |
MAELEZO |
Ushirikiano |
Tunathamini juhudi za pamoja na shirikishi ili kufikia lengo moja na kuwaridhisha wadau wetu. |
Uadilifu |
Tunafanya uamuzi wa kuwajibika kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma, utu na uaminifu |
Ubunifu |
Tunahimiza ubunifu na mabadiliko ya mtazamo katika utoaji wa huduma |
Uwajibikiaji |
Tunajitolea kuchukua jukumu na umiliki wa vitendo/hatua za mtu binafsi au timu kwa njia ya uwazi |
Bidii |
Tunazingatia matokeo yenye kuleta mageuzi, uthabiti, sahihi na kutumia mbinu bora. |
Ujumuishaji |
Tumejitolea kuzingatia na kudumisha kanuni za usawa na haki. |