MAONI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amewataka Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji maoni kwa ajili ya kupata maudhui ya kutumika kuandika Dira ya Taifa 2050.
Ametoa rai hiyo leo Agosti 28, 2024, ofisini kwake Mjini Magharibi wakati akiongea na wajumbe wa Tume ya Mipango na Timu Kuu ya Kitaalamu ya Dira ya Taifa 2050 iliyoongozwa na mjumbe wa Tume ya Mipango na Mwenyekiti wa Timu hiyo, Dkt. Asha Rose Migiro.
Vile vile amehimiza ulazima wa kila Mtanzania kuhakikisha anadumisha amani na utulivu ili mipango ya maendeleo ya Dira 2050 iweze kutekelezwa kikamilifu.