Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI - GEITA
Geita, 11 Julai 2024 - Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani kimeadhimishwa kitaifa leo katika Kituo cha Maonyesho cha Kibiashara (EPZA), Bombambili, Mkoani Geita, yakiongozwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo. Maadhimisho haya, yanayofanyika kila mwaka kimataifa tangu idadi ya watu duniani ilipofikia bilioni tano tarehe 11 Julai 1989, yamekuwa yakiadhimishwa na Tanzania kitaifa tangu kujiunga na Umoja wa Mataifa. Serikali kupitia Tume ya Mipango, ikishirikiana na UNFPA na mashirika ya kiraia, husherehekea siku hii ili kupata takwimu sahihi zitakazosaidia katika uandaaji wa mipango na mikakati ya maendeleo yenye usawa.