Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO KUHUSU RASIMU YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
11 Jan, 2025
MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO KUHUSU RASIMU YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kupitia Tume ya Taifa ya Mipango imeratibu mkutano muhimu wa wadau wa maendeleo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Dar es Salaam Leo tarehe 10 Januari 2025.

Mkutano huu uliwaleta pamoja mashirika ya Umoja wa Mataifa, balozi mbalimbali, na mashirika ya kimataifa kwa lengo la kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, aliongoza majadiliano huku Dkt. Mursali Milanzi akitoa utangulizi.

Wadau walipongeza juhudi za Serikali na kubainisha kuwa Rasimu ya Dira 2050 inazingatia maendeleo jumuishi, ustawi wa makundi yote, uimarishaji wa uchumi, na masuala ya mazingira.

Watanzania wanahimizwa kuendelea kushiriki katika mchakato huu muhimu kwa maendeleo endelevu ya Taifa.