RASIMU YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 YAPITIWA NA WAFANYABIASHARA NA WAMILIKI WA MAKAMPUNI
11 Jan, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) leo amekutana na baadhi ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Makampuni Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhakiki na kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mkutano huu ni sehemu ya jitihada za kuboresha Dira ya Taifa ya Maendeleo ili kuhakikisha inakisi maoni, maono, na matarajio ya kila Mtanzania kuelekea Tanzania tunayoitaka.
Prof. Mkumbo amepongeza ushiriki wa sekta binafsi katika mchakato huu na kusisitiza umuhimu wa maoni yao katika kufanikisha mwelekeo wa maendeleo ya Taifa kwa miaka 25 ijayo.