Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI KUPITIA TUME YA MIPANGO YA TAIFA YAANDAA WARSHA ELEKEZI KUHUSU MPANGO WA MUDA MREFU (LTPP)
11 Jan, 2025
OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI KUPITIA TUME YA MIPANGO YA TAIFA YAANDAA WARSHA ELEKEZI KUHUSU MPANGO WA MUDA MREFU (LTPP)

Tume ya Mipango ya Taifa, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb) amefungua warsha elekezi ya siku mbili inashoshirikisha wadau mbali mbali wa Maendeleo kuhusu Mpango wa Muda Mrefu wa Maendeleo (LTPP) katika Vituo vya Mikutano vya APC, Bunju, Dar es Salaam, kuanzia leo tarehe 5 Januari 2025.

Warsha hii inalenga kutathmini utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa (TDV) 2025, kushiriki mafanikio makuu, kujifunza changamoto zilizojitokeza, na kutoa ujumbe wa kina kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Washiriki watapata fursa ya kuelewa malengo, madhumuni, na majukumu ya mifano inayotumika kutoa mwongozo wa Dira ya 2050 na maendeleo ya LTPP 2050. Warsha hii ni hatua muhimu katika kukuza ushirikiano na kuimarisha mipango ya maendeleo ya taifa, ili kufikia mustakabali bora zaidi kwa Watanzania wote.