Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

WARSHA YA UELEWA WA MPANGO WA MAENDELEO WA MUDA MREFU (LTPP) YAFANYIKA KWA SIKU YA PILI.
11 Jan, 2025
WARSHA YA UELEWA WA MPANGO WA MAENDELEO WA MUDA MREFU (LTPP) YAFANYIKA KWA SIKU YA PILI.

Tume ya Mipango ya Taifa leo tarehe 7 Januari 2025 imeendelea na warsha kwa wadau mbali mbali wa Maendeleo nchini ya kuimarisha uelewa wa Mpango wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP) kwa siku ya pili, warsha hii imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa APC, Bunju, Dar es Salaam.

Warsha hii imejikita katika mafunzo ya kivitendo kuhusu upangaji wa vipaumbele kwa kuzingatia takwimu zilizopo, matumizi ya mbinu bora za kupanga, na mijadala shirikishi inayowezesha washiriki kubadilishana uzoefu na maarifa.

Vilevile, vikundi vya washiriki vimejifunza kutoka kwa uchambuzi wa kina wa sekta mbalimbali chini ya mpango wa Big Results Now (BRN). Hatua hii inalenga kuimarisha uwezo wa timu ya LTPP katika kutumia ushahidi wa kitaalamu na takwimu sahihi katika kupanga mipango endelevu kwa maendeleo ya taifa.