Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

SEMINA ELEKEZI KWA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA NCHI MBALIMBALI KUELEKEA ZOEZI LA UKUSANYAJI MAONI YA WANANCHI NA WADAU KUHUSU DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO
08 May, 2024
SEMINA ELEKEZI KWA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA NCHI MBALIMBALI KUELEKEA ZOEZI LA UKUSANYAJI MAONI YA WANANCHI NA WADAU KUHUSU DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO

Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wamekutana na timu kuu ya kitaalamu ya uandishi wa Dirara ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kujadili maandalizi na mikakati ya ushishwaji wa wadau kuhusu maandalizi ya Dira hiyo. 

Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 25 Aprili, 2024. Kikao hicho kililenga kuimarisha ushirikiano na kukusanya maoni kutoka kwa jamii ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Lengo ni kuhakikisha kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inajumuisha mitazamo na matarajio ya pande zote, wakiwemo wanaoishi ndani na nje ya Tanzania.