SEMINA YA WAKUU WA MIKOA 17 APRILI, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) amesema kuwa semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo viongozi hao kwenye mambo makuu matatu.
Prof. Mkumbo amesema jambo la kwanza, ni kuhusu mchakato wa maandalizi ya Dira 2050 ikiwemo mbinu na nyenzo za ushirikishaji wadau zitakazotumika.
Aidha, la pili lililenga kuwaelimisha kuhusu wajibu na majukumu yao katika uhamasishaji umma, usimamizi na uratibu wa ukusanyaji maoni kwenye maeneo yao.
La mwisho lilihusu kuwataarifu na kuwapatia orodha ya maeneo ya kijografia (Wilaya, Halmashauri, Kata/Shehiya, Mitaa/Vijiji na Vitongoji) yaliyoainishwa kwa ajili ya ukusanyaji maoni katika ngazi ya kaya, pamoja na taratibu mahsusi zitakazotumika katika kipindi chote cha ukusanyaji maoni katika maeneo yao ya kiutawala.
Awali, akitoa salamu za utambulisho Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida, alieleza hatua mbalimbali kuhusu mchakato wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na zaidi zilizohusisha tangu mchakato huo ulipoanza 2021 hadi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipozindua mchakato wa ukusanyaji wa maoni Disemba 9, 2023 na hatua mbalimbali zilizofikiwa hadi kufikia semina hiyo kwa wakuu wa Mikoa.
Vile vile, viongozi mbalimbali wa kitaifa, Waheshimiwa Mawaziri, Makatibu Wakuu, kutoka pande zote za Muungano, walipata fursa ya kutoa salamu za katika semina hiyo.