Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Mipango

BARAZA LA PILI LA WAFANYAKAZI TUME YA TAIFA YA MIPANGO
11 Jan, 2025
BARAZA LA PILI LA WAFANYAKAZI TUME YA TAIFA YA MIPANGO

Dodoma, Disemba 21, 2024 – Tume ya Taifa ya Mipango imemaliza mwaka kwa mafanikio kwa kufanya mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi tangu kuanzishwa kwake. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma chini ya uongozi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), akishirikiana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume, Dkt. Mursali Ally Milanzi.

Kwa kauli mbiu isemayo “Utendaji kazi wa pamoja unaozingatia weledi na uadilifu ni chachu katika ustawi wa Taasisi,” baraza hilo lililenga kuimarisha mshikamano, uwajibikaji, na utendaji bora ndani ya Tume.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Mhe. Nyongo aliwasihi wafanyakazi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao, akisisitiza kuwa mafanikio ya taasisi yanategemea juhudi za pamoja na nidhamu ya hali ya juu.

Baraza hilo limehitimishwa kwa kutoa maazimio muhimu ya kuimarisha utendaji kazi wa Tume katika mwaka ujao, likibeba matumaini makubwa ya kukuza mchango wa Tume katika maendeleo ya Taifa.