TUME YA MIPANGO YATOA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO NA UELEWA JUU YA KUAINISHA VIPAUMBELE VYA TAIFA (NKRAs)
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango amefungua Mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa juu ya juu ya kuainisha vipaumbele vya Taifa Leo Tarehe 6 Mei, 2024, Takwimu House, Dodoma.
Mafunzo hayo yalongozwa na wajumbe kutoka taasisi ya Pemandu yakiwa yamelenga katika kuwajengea uwezo watumishi wa sekta mbali mbali ili kuainisha vipaumbele katika kuelekea katika malengo ya Nchi kujijenga kiuchumi utakao akisi dhima ya Dira ya Taifa ya Maendeleo na kuweza kuvipa kipaumbele katika maandaliza ya bajeti zao.
Mafunzo haya yanawakutanisha wadau mbalimbali katika kujadili na kubainisha vipaumbele vya Taifa. Lengo kuu lilikuwa ni kutoa uelewa na kujenga uwezo wa namna bora ya kuainisha vipaumbele ili kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika utekelezaji wa vipaumbele na programu za miradi ya maendeleo, kwa lengo la kuleta matokeo tarajiwa katika mageuzi ya uchumi wa Taifa letu.
Vile vile Kikaokazi kinafanyika chini ya usimamizi wa Tume ya Mipango, ambayo kupitia kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Tume ya Mipango Na. 1 ya Mwaka 2023, imepewa jukumu la kusimamia uchumi, mchakato wa upangaji, na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa. Kifungu hicho pia kinatoa mamlaka ya kufuatilia utekelezaji wa maeneo muhimu ya vipaumbele vya Taifa kwa sekta mbalimbali za uchumi, na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kutatua changamoto zozote zitakazobainika.
Washiriki wanapata fursa ya kujadili kwa kina namna bora ya kuzingatia maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Kikaokazi hicho pia kilijadili kwa mapana suala la uhamisho wa matumizi ya fedha na mapungufu katika mfumo wa upangaji na uwekaji wa vipaumbele katika mipango na bajeti ya maendeleo. Wadau wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuainisha vipaumbele ili kuleta matokeo chanya katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Taifa.