Hotuba ya Bajeti 2024/2025, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji | 18 Aprili, 2024
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI
HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS -
MIPANGO NA UWEKEZAJI, MHESHIMIWA PROF. KITILA ALEXANDER MKUMBO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI KWA MWAKA 2024/25
DODOMA APRILI 2024
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb.)
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji
Dkt. Tausi Mbaga Kida
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji
YALIYOMO
2. MAJUKUMU YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI
3. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2023/24
3.1. MWENENDO WA MAPATO NA MATUMIZI HADI MACHI, 2024 (FUNGU 11, FUNGU 07 NA FUNGU 66)
3.2. MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA VIPAUMBELE KWA MWAKA 2023/24
3.3. HALI NA MWENENDO WA UWEKEZAJI NCHINI
3.4. UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UWEKEZAJI WA SEKTA BINAFSI
3.5. UANZISHWAJI NA UENDELEZAJI WA MAENEO MAALUM YA KIUCHUMI NA MIRADI YA KIMKAKATI
4. MPANGO NA BAJETI YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI KWA MWAKA 2024/25
4.1 VIPAUMBELE NA KAZI ZITAKAZOTEKELEZWA KWA MWAKA 2024/2025
4.2 Vipaumbele vya Mpango na Bajeti kwa Taasisi
4.2.1 Ofisi ya Msajili wa Hazina
4.2.3 Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA)
4.2.4 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
ORODHA YA VIFUPISHO
4R |
Reconciliation, Reform, Resilience and Re-building |
AZAKI |
Asasi za Kiraia |
BAKWATA |
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania |
BASUTA |
Baraza la Sunnah Tanzania |
BEU |
Business Environment Unit |
BITs |
Bilateral Investment Treaties |
BRELA |
Business Registration and Licensing Authority |
CCM |
Chama Cha Mapinduzi |
CCT |
Christian Council of Tanzania |
CTI |
Confederation of Tanzania Industries |
DLsw |
Dealer’s Licenses |
EACOP |
East African Crude Oil Pipeline |
EFD |
Eletronic Fiscal Devices |
EPZA |
Economic Processing Zones Authority |
EPZA |
Economic Processing Zones Authority |
FCS |
Foundation for Civil Society |
FCS |
Foundation for Civil Society |
FDI |
Foreign Direct Investement |
GCLA |
Government Chemist Laboratory Authority |
IACA |
International Apprecenticeship & Competency Academy |
IACA |
International Apprecenticeship & Competency Academy |
LNG |
Liquified Natural Gas |
LNG |
Liquified Natural Gas |
MLs |
Mining Licenses |
MoU |
Memorandum of Understanding |
MoU |
Memorandum of Understanding |
NACSAP |
National Anti-Corruption Strategy and Action Plan |
NEMC |
National Environment Management Council |
NIDA |
National Identification Authority |
OMH |
Ofisi ya Msajili wa Hazina |
OR-MU |
Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji |
OR-TAMISEMI |
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa |
OSHA |
Occupational Safety and Health Authority |
OTRMIS |
Office of the Registrar Management Information System |
PCLs |
Processing Licenses |
PIC |
Public Investment Centre |
PLs |
Prospecting Licenses |
PMLs |
Primary Mining Licenses |
SBT |
Sugar Board of Tanzania |
SDGs |
Sustainable Development Goals |
SEZ |
Special Economic Zone |
SOP |
Standard Operating Procedures |
SOP |
Standard Operating Procedures |
TANESCO |
Tanzania National Electric Supply Company |
TANROADS |
Tanzania National Roads Agency |
TBS |
Tanzania Bureau Standards |
TCCIA |
Tanzania Chamber of Commerce, Industry & Agriculture |
TCRA |
Tanzania Communications Regulatory Authority |
TEC |
Tanzania Epistical Council |
TEF |
Tanzania Editors’ Forum |
TEHAMA |
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano |
TeIW |
Tanzania Electronic Investment Window |
TFDA |
Tanzania Food and Drugs |
TIC |
Tanzania Investment Centre |
TMDA |
Tanzania Medicines and Medical Devices Authority |
TMDA |
Tanzania Medicines and Drugs Authority |
TPSF |
Tanzania Private Sector Foundation |
TRA |
Tanzania Revenue Authority |
TTMS |
Telecommunication Traffic Monitoring System |
UAE |
United Arab Emirates |
UKIMWI |
Upungufu wa Kinga Mwilini |
ORODHA YA MAUMBO
Umbo 1: Asilimia ya Miradi Iliyosajiliwa TIC Kisekta 2021-2023.
Umbo 2: Wastani wa Idadi ya Miradi ya Uwekezaji Iliyosajiliwa na TIC kwa Mwaka kwa Awamu za Uongozi.
Umbo 5: Miradi Iliyosajiliwa TIC kati ya Mwaka 2020 na 2023
1. UTANGULIZI
- Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja kwamba kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Bunge lako lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa Mwaka 2023/24 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji (Fungu 11); Ofisi ya Msajili wa Hazina (Fungu 07); na Tume ya Mipango (Fungu 66) kwa Mwaka 2024/25.
- Mheshimiwa Spika, ninamshukuru Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema iliyoniwezesha kuwasilisha Hotuba hii kwa mara ya kwanza nikiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji (OR-MU). Aidha, ninamshukuru Mungu kwa kulijalia Taifa letu amani, utulivu na mshikamano na kwa kutuwezesha kukutana katika mkutano huu wa 15 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujadili namna ya kuharakisha maendeleo ya Taifa kupitia Bajeti zinazowasilishwa katika Bunge hili la Bajeti.
- Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nitumie nafasi hii kutoa pole kwako, waheshimiwa wabunge na wananchi wote kwa ujumla kwa msiba uliolipata Bunge kufuatia kufariki kwa Mheshimiwa Ahmed Yahya Abdulwakil, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani. Tunamuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina! Aidha, nitumie nafasi hii, kwa niaba ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na taasisi za umma inazozisimamia kutoa pole kwa wananchi wote waliokumbwa na mafuriko yaliyojitokeza katika msimu huu wa mvua katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
- Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa, ninapenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri, pamoja na juhudi za dhati alizoziweka katika kuiendeleza nchi yetu ili tuweze kufikia malengo tuliojiwekea. Kipekee, na kwa muktadha wa majukumu ya Ofisi yangu, ninampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuimarisha diplomasia ya uchumi iliyochochea kuongezeka kwa mashirikiano baina ya nchi yetu na nchi mbalimbali rafiki, kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuitangaza nchi yetu kuwa kivutio na mahala salama katika uwekezaji. Aidha, ninamshukuru Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uongozi wake makini na jitihada zake kubwa katika kuendelea kuijenga Zanzibar yenye maendeleo makubwa.
- Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Dotto Mashaka Biteko (Mb.), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, kwa kazi kubwa wanazofanya katika kumsaidia Mheshimiwa Rais kuendesha nchi yetu vyema.
- Mheshimiwa Spika, ninawapongeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria chini ya uongozi mahiri na imara wa Mwenyekiti wake Mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama, Mbunge wa Jimbo la Madaba na Makamu wake Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Jimbo la Nkenge, kwa ushirikiano, maelekezo, maoni na ushauri mzuri walioutoa wakati wa kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2023/24 na Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/25.
- Mheshimiwa Spika, ninawapongeza waheshimiwa wabunge waliopata heshima ya kuteuliwa na kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika Serikali na Bunge letu tukufu. Hawa ni: Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Zainabu Athuman Katimba (Mb) kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) na Mheshimiwa Daniel Baran Sillo (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Ninampongeza Mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama, Mbunge wa Jimbo la Madaba, na Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, kwa kuchaguliwa kuwa wenyeviti wa Bunge.
- Mheshimiwa Spika, ninawashukuru viongozi wenzangu katika Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, kwa ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu yetu na kwa maandalizi mazuri ya Hotuba hii. Hawa ni pamoja na Dkt. Tausi Mbaga Kida (Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji), Ndugu Lawrence Nyasebwa Mafuru (Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango), Ndugu Nehemiah Kyando Mchechu (Msajili wa Hazina), Ndugu Charles Jackson Itembe (Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje), na Ndugu Gilead John Teri (Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania). Aidha, ninawashukuru Menejimenti na watumishi wote wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu.
- Mheshimiwa Spika, kwa umuhimu wa pekee kabisa, ninawashukuru sana wananchi wenzangu wa Jimbo la Ubungo kwa kuendelea kunipa ushirikiano na imani wakati wote ninapoendelea kuwawakilisha. Ninaahidi kuendelea kuwatumikia kwa juhudi na maarifa ili kuhakikisha jimbo letu linaendelea kupata maendeleo.
- Mheshimiwa Spika, pamoja na utangulizi nilioutoa hapo juu, Hotuba yangu ina sehemu kuu tatu: Majikumu ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji; Taarifa ya Utekelezaji wa kazi zilizofanyika kwa Mwaka 2023/24; na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2024/25.
2. MAJUKUMU YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ilianzishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 407 (A na B) la tarehe 22 Juni, 2023. Ofisi hii ina jukumu la msingi la kuandaa na kuratibu utekelezaji wa sera, sheria na mikakati inayohusu mipango ya maendeleo ya Taifa, uwekezaji, kusimamia utendaji wa mashirika ya umma, na kuratibu utekelezaji wa mikakati ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.
- Mheshimiwa Spika, Majukumu mahususi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ni haya yafuatayo:-
- Kubuni na kusimamia utekelezaji wa sera kuhusu Mipango na Uwekezaji nchini;
- Kuratibu na kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi;
- Kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara;
- Kuratibu taasisi za kitaifa na kimataifa zinazohusika na uwekezaji; na
- Kuzisimamia taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ambazo ni Tume ya Mipango, Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA) na Kituo cha Uwezekezaji Tanzania (TIC).
- Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2024, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji ina jumla ya watumishi 80 katika taaluma na kada mbalimbali waliogawanywa kufanya kazi katika idara nne na vitengo saba.
3.1.1 Makusanyo ya Maduhuli
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Fungu 07 - Ofisi ya Msajili wa Hazina iliidhinishiwa kukusanya maduhuli yenye jumla ya shilingi trilioni 1.07. Maduhuli hayo yanatokana na gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi ya taasisi zinazochangia, mrejesho wa Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTMS), rejesho la riba na mikopo, ziada na malipo mengineyo. Hadi kufikia Machi, 2024, jumla ya shilingi bilioni 459.44 sawa na asilimia 74.11 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 619.96 kwa kipindi kinachorejewa zilikusanywa, sawa na asilimia 42.96 ya lengo la mwaka. Matarajio ni kuwa sehemu kubwa ya makusanyo itapatikana katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2023/24.
3.1.2 Bajeti iliyoidhinishwa
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Mafungu matatu (3) ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji yaliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 126.19 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 15.61 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 79.90 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi bilioni 30.69 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
3.1.2 Matumizi
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi 2024, mafungu matatu (3) ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji yamepokea na kutumia jumla ya shilingi bilioni 68.08 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo sawa na asilimia 53.95 ya kiasi kilichoidhinishwa. Kati ya kiasi kilichopokelewa, shilingi bilioni 8.48 nikwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni 41.83 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi bilioni 17.76 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
- Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa maeneo ya vipaumbele kwa mafungu matatu (3) ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ni kama ifuatavyo: -
- Kuandaa Dira 2050 na Mpango Mkakati wa Muda Mrefu
- Mheshimiwa Spika, Ajenda ya Maendeleo ya Taifa imefafanuliwa na inaongozwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 ambayo utekelezaji wake utafika ukomo Juni, 2026. Kwa msingi huo, Serikali imeanza maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inatarajiwa kutoa mwongozo na mwelekeo wa maendeleo ya nchi kwa kipindi cha miaka 25.
- Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2024 shughuli zifuatazo zimefanyika katika maandalizi ya Dira:
- K